Toleo Jipya
Toleo Wiki Jana
Tuwasiliane
  

CCM na CUF kamilisheni kazi mloianza

TAHARIRI
  • CCM na CUF heshimuni kazi yenu
  • CCM na CUF rudini mezani haraka

Toleo Na. 097

Na Saed Kubenea
MAKAMPUNI ya kuzalisha umeme ya Richmond na Dowans yanamilikiwa na mtu mmoja. Taarifa ndani ya serikali imekiri pia kwamba hayo ni makampuni ya mfanyabiashara mmoja mashuhuri raia wa Tanzania...
Tahariri
MAZUNGUMZO ya kutafuta muwafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) yanaendelea kukwama. Kukwama kwa mazungumzo hayo kumetokana na misimamo iliyowekwa na vyama hivi...
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingia kijijini Ubungo Msewe kwa kutaka ripoti kamili ya ufuatiliaji tuhuma mbalimbali zilizofikishwa kwake, MwanaHALISI imefahamishwa...
Na Ndimara Tegambwage
WIKI iliyopita kulikuwa na taarifa katika vyombo vya habari juu ya vijana waliokamatwa kwa madai ya “kumtukana” rais mstaafu Benjamin Mkapa. Lakini habari hizo hazikusema ni matusi yapi alitukanwa...
Na Iddy Mkwama
HABARI za kuwapo ufisadi uliokithiri ndani ya Shirika la Bima la Taifa (NIC), si ngeni na hazishangazi kwa wengi hasa wale wanaofuatilia mwenendo wa shirika hilo...
NI lazima uwe na shahada ya falsafa ili ukielewe vema Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kudhihirisha kwamba chama tawala ni dude lisiloweza kueleweka...
Na Ndimara Tegambwage
NANI anataka kuona askari polisi na askari magereza wakifanya maandamano na migomo wakidai serikali iwasikilize na kuwalipa mishahara inayolingana na kazi yao? Nani?
ANAKABILIWA na changamoto nyingi kama msomi binafsi, ila ana changamoto mahsusi kama kiongozi wa taasisi nyeti. Wala hakujua angeongoza moja ya taasisi alizoziakisi baada ya kutakiwa kubuni mfumo mpya wa uendeshaji mamlaka za kusimamia utoaji huduma kwa umma...
Na Stanislaus Kirobo
HAKUNA ubishi kuwa “ufisadi” ni neno lililochukua nafasi kubwa zaidi magazetini katika awamu hii ya uongozi wa nchi kuliko huko nyuma...
Na Saed Kubenea
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya tano ya Baraza la Mawaziri tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi, takribani miaka miwili na nusu iliyopita...
Na Joseph Mihangwa
NIMEPOKEA maswali mengi na hoja mbalimbali kutoka kwa wasomaji wa gazeti hili kutokana na makala yangu iliyochapishwa katika toleo la 30 Aprili 2008 iliyobeba kichwa cha habari kisemacho: “Karume na zimwi la Mapinduzi”...
INASIKITISHA sana kuona jitihada zilizochukuliwa na vyama viwili hasimu katika siasa za Zanzibar, zimeishia...
"Si Bure, Yussuf Manji ana lake Yanga." Ndivyo ninavyolazimika kuamini kutokana na mambo kadhaa yaliyojitokeza tangu bilionea huyo alipotia mguu Yanga mwaka 2006...

MAZUNGUMZO ya kutafuta muwafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) yanaendelea kukwama.

Kukwama kwa mazungumzo hayo kumetokana na misimamo iliyowekwa na vyama hivi.

Wakati CUF wanasema mazungumzo yamemalizika, na kwamba ajenda ya kura ya maoni ililetwa kwa hila na CCM, wenzao wanasema mpaka sasa ni ajenda nne tu zilizojadiliwa.

Ajenda hii, kwa mujibu wa CCM, inahusu utaratibu wa utekelezaji na progamu ya utekelezaji wa makubaliano.

Pande zote mbili tumezisikia. Tumewasikia CCM kama tulivyowasikia CUF. Lakini ukweli uliobaki ni kwamba mazungumzo haya yamekwama kutokana na ulaghai wa CCM wa kuumba jambo jipya walilolipachika jina la “kura ya maoni”.

CCM wanakiri kuwa hili halikuwamo katika vikao vyote 14 vilivyokwisha fanyika.

Kwa mujibu wa waraka wa CCM uliofikishwa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC), jambo hili lililetwa na Kamati ya CCM katika mazungumzo, baada ya kutakiwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume waliingize.

Hakika, hili ndilo chimbuko na kichocheo kikuu cha muwafaka kukwama.

Matokeo yake, ni kupanda kwa joto la kisiasa Zanzibar maana tunaanza kusikia yaliyopita yakifanana na yale yaliyotokea baada ya kumalizika chaguzi za mwaka 995 na 2000.

Ni vema CCM ikaondoa ajenda hii ya kura ya maoni kwa maslahi ya taifa, ili vyama virudi kumalizia palipobaki.

Ni imani yetu hilo linawezekana. Hii ni kwa sababu katu CCM haiwezi kujivua na lawama za kuchochea upya mgogoro ambao mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, aliuahidi ulimwengu kuupatia ufumbuzi wa kudumu.

Ikumbukwe kwamba CCM ndio chama tawala na kinacholaumiwa katika kukataa kuachia mkondo wa demokrasia kufuatwa.

Kama Watanzania wanataka ukweli ubaki kuwa ukweli, basi CCM hawana jeuri ya kutamba kuwa wamefanikiwa kusimamia uchaguzi huru na wa haki Zanzibar.

Kinachoshuhudiwa kila unapofanyika uchaguzi, tangu wa 1995, ni vurugu na ukiukaji wa misingi ya uchaguzi unaonyima wananchi fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Binadamu wenye akili wakifika mahali kuamua na kusimamia hasa kukwamisha kile wanachokiamini kitaleta ufumbuzi wa mgogoro, basi hapo tumeondokana na ubinadamu. Tunaweza kwenda hivi?