Toleo Jipya
Toleo Wiki Jana
Tuwasiliane
  

Rais Kikwete chukua nafasi

TAHARIRI

Toleo Na. 098

Tahariri
KATIKA safu hii wiki iliyopita, tulitaka vyama vya CCM na CUF virudi mezani ili kukamilisha mchakato wa utekelezaji wa muafaka uliofikiwa baada ya miezi 14 ya majadiliano...
Na Saed Kubenea
“HUU si ushindi wangu binafsi, bali ni ushindi wa Watanzania. Ni ushindi wa wazalendo wa nchi hii, dhidi ya mafisadi. Hakika, huu ni ushindi wa wananchi wazalendo wa kweli katika taifa lao"...
Na Jabir Idrissa
ZIPO fitna tatu kuu kwa sasa zinazohusiana na hali ya mambo ilivyo Zanzibar kisiasa kiasi cha kukumbusha mabaya yaliyotokea mara tu baada ya uvurugaji matokeo ya uchaguzi mkuu wa 1995 na 2000...
Na Stanislaus Kirobo
Tangu ateuliwe kushika wadhifa wa Uwaziri Mkuu takriban miezi mitatu iluiyopita, Mizengo Pinda amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika shughuli za nje ya nchi mara tatu. Kwa wastani amefanya hivyo mara moja kila mwezi...
Na Joseph Mihangwa
HAKIKA, Zanzibar inaumwa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kama kuna maneno sahihi ya kuelezea kiwango cha ugonjwa wake, ni kwamba “Zanzibar sasa imo katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)...
Na Mbasha Asenga
KUNA uvumi uliotamalaki kwamba ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lipo kundi la watu linalojiandaa kumpinga rais wao mwaka 2010....
Na Saed Kubenea
KATIKA siku za karibuni, mmoja wa wanasiasa wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Job Lusinde, ametoa kauli kwamba watuhumiwa wa ufisadi wenye nyadhifa ndani ya chama hicho wavuliwe uwanachama...
Na Mwandishi Wetu
KAMA kuna jambo ambalo baadhi ya Watanzania wenzetu hawajafuzu, ni mwenendo wa siasa za ushindani zinazohusisha chama tawala na vyama vya upinzani...
Na Fareed Zakaria
Mwezi uliopita kura moja mpya ya maoni ilionyesha kwamba asilimia 81 ya Wamarekani wanaamini kwamba nchi yao iko katika mwelekeo usio sahihi...
Na Bakari Makusudi
KUONDOKA nchini Tanzania kwa uongozi wa juu wa kikundi pekee cha waasi kinachoendeleza vita dhidi ya serikali ya Burundi inayoongozwa na kilichokuwa kikundi cha waasi cha CNDD-FDD kunafungua ukurasa mpya kisiasa nchini Burundi....

KATIKA safu hii wiki iliyopita, tulitaka vyama vya CCM na CUF virudi mezani ili kukamilisha mchakato wa utekelezaji wa muafaka uliofikiwa baada ya miezi 14 ya majadiliano.

Lakini wakati tukihimiza hilo, tunasikitika kuona wanatokea watu wanatoa kauli zinazodisha malumbano na kuchochea chuki na uhasama dhidi ya viongozi wa CUF.

Hawa si wengine, bali ni viongozi waandamizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) na  kitengo cha propaganda cha chama hicho.

Kila mmoja anajua kwamba Zanzibar kuna tatizo kubwa la kisiasa. Kama tunataka kutazama mambo kwa maslahi ya taifa, basi hakuna anayebisha.

Na hilo ndilo lililomsukuma Rais Jakaya Kikwete kumaliza tatizo alipoahidi kutafuta njia ya “kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa Zanzibar.”

Ahadi hiyo ilihalalisha kuanza mchakato wa majadiliano. Ni wazi CCM na CUF vimeshaafikiana, isipokuwa, tofauti zimekuja katika namna ya kutekeleza yale yaliyokubaliwa.

Katika hali kama hiyo, hatudhani kama ni busara kutokea Watanzania, tena viongozi wa juu wa CCM, wakathubutu kutoa kauli za kejeli, chuki na uhasama, dhidi ya CUF na rais kwa ujumla.

Kusema kwamba CCM kukubali kukaa mezani na CUF ni fadhila tu kwa chama cha upinzani na kwamba Rais Kikwete hana uwezo wa kumaliza mgogoro huo bila ya kushirikisha vikao vya chama chake, ni dharau kwake na kubeza kile anachokisimamia.

Rais anayo mamlaka tena makubwa, hasa ukizingatia kwamba alipotoa ahadi ile aliitoa kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadaye amekuja kuvikwa na uenyekiti wa taifa wa chama chake. Hayo ni mamlaka.

Anajua vizuri sababu ya kuahidi alichoahidi. Anajitambuwa kwamba kuwa kwake kiongozi wa ngazi ya juu nchini kwa muda mrefu kumempatia uzoefu wa kutosha wa kuujua mgogoro wa Zanzibar na athari zake.

Tukubaliane kuwa hali ya kuaminiana, japo kwa kiwango kidogo, iliyokuwepo kwa Kamati mbili za mazungumzo, imetoweka na msimamo wa CUF kutotaka tena kukaa na CCM, ni ushahidi tosha kwamba bado Zanzibar inasumbuliwa na mgogoro na lazima umalizwe.

Sawa, hawawezi kukaa tena na CCM, lakini na umma hauwezi kuendelea kuona nchi inarudi katika machafuko kama ilivyokuwa huko nyuma. Tunataka wote wanaohusika kuheshimu matakwa ya wananchi na muafaka uheshimiwe na kusainiwa haraka iwezekanavyo.

Katika hili, hatuoni njia ya kupita, isipokuwa Rais Kikwete kuchukuwa nafasi yake kama kiongozi mkuu wa taifa, kuelekeza na kuagiza cha kufanywa kwa maslahi ya taifa. Lazima tuondoke tulipo na twendeni mbele!